HabariNews

Maradhi ya macho yaendelea kutatiza Wakaazi Mombasa

Zaidi ya watu elfu moja kaunti ya Mombasa wanaugua maradhi ya macho mekundu yaliyoripotiwa kuzuka katika kaunti hii.

Idara ya Afya kaunti ya Mombasa imethibitisa hilo huku ikibaini kuwa idadi hiyo huenda ikawa ni kubwa zaidi kutokana na baadhi kuwa hawajafika katika vituo vya afya.

Idara hio iliendelea kutoa tahadhari kwa wakaazi wote na hasa wazazi kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo.

Kulingana na Afisa wa Afya kaunti ya Mombasa Abdallah Deleno, watoto na watu wazima ni miongoni mwa waathiriwa.

Deleno aliwataka wakazi kutokuwa na hofu akiyataja maradhi hayo kuwa ya kawaida japo akitoa himiza ya kuchukua tahadhari ili kujilinda na maradhi hayo ikiwemo kudumisha usafi kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni na kujizuia kushika macho kila mara.

“ huu ugonjwa wa macho ni kweli umetokea na ni jambo tu la kawaida ambalo limeathiri watoto na watu wazima. nafikiri inaweza fika zaidi ya 1000, watu ni wengi kuna wengine ambao labda hawajajitokeza lakini wale wamefika hospitani ni wengi”.

Afisa huyo wa afya hata hivyo aliwataka wakazi kufika katika kituo cha afya kilicho karibu iwapo yeyote atahisi dalili za ugonjwa huo.

Kuzuia ugonjwa usiwe unasambaa kwa mitaa ama kwa kijiji ama kwa nyumba yenyewe , watu waongezzze tu hali ya unadhifu na kila kitu itakua sawa na iwapo kuna mtu anaona macho imeanza kuwana uchafu inatoa discharge aende tu hospitali na anaweza tibiwa na akawa sawa

Katika kaunti ya Kilifi, maafisa wa Afya waliripoti visa kadhaa vya ugonjwa huo, hata hivyo wakiwataka wakazi kutokuwa na hofu bali wazingatie viwango vya usafi kwa kunawa mikono yao kwa maji na sabuni.

Peter Mwarogo, ni Waziri wa afya kaunti ya Kilifi,  na alisema kuwa haina haja ya kuwa na hofu kwani ugonjwa huo ni wa kawaida na walishawai kurekodi kesi nyingi za ugonjwa huu hapo awali.

Mkurupuko huu uliripotiwa awali katika nchi jirani ya Tanzania mnamo Disemba ambapo inaonekana kusambaa haraka haswa katika miji iliopo mkoani mwa pwani.

Maambukizi ya Ugonjwa wa Macho Mekundu ambao kitaalam huitwa Conjunctivitis husababishwa na virusi, bakteria, vizio au viwasho.

Dalili za maambukizi ni pamoja na jicho au macho kuwasha, kuvimba Ngozi nyembamba iliyo wazi ya sehemu nyeupe ya jicho na ndani ya kope, na kuongezeka kwa machozi na matongo.

BY NEWS DESK