HabariMazingiraNews

TUUNGANE KATIKA VITA DHIDI YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA – VIONGOZI WA KIDINI

Viongozi wa mataifa ya bara la Afrika wametakiwa kusimama pamoja na wananchi katika kupinga utumizi wa bidhaa zinazoharibu mazingira nchini Kenya na bara Afrika kwa ujumla.

Haya ni kwa mujibu wa Viongozi wa kidini, watetezi wa mazingira na mashika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika.

Wakiongea wakati wa uzinduzi wa afisi za shirika la kupambana na Mabadailiko ya tabia nchi ya GreenFaith Afrika jjini Nairobi, Mkurugenzi wa hamasisho katika shirika Hilo, Meryne Warah, ametaka serikali kuwashirikisha washikadau wote katika vita hivyo, Ili kuepusha mataifa kutumbukia katika janga la madhara ya tabia nchi.

Kwa upande wake Salim Bayani akiongoza Viongozi wa kidini nchini, amewataka wananchi kichhukua kujumu la usafi wa mazingira mkononi mwao, kwani juhudi hizo huanza mashinani.

Wakati uo huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la GreenFaith Fletcher Harper, ameyataka mataifa ya bara la Afrika kutumia raslimali walizonazo katika kuepuka machafuzi yanayosababishwa na kampuni mbalimbali zinazoharibu mazingira.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali Afrika ikiwemo,
Ghana, Nigeria, Congo, Tanzania, Uganda and the DRC

By Editorial Desk