HabariNews

HAKI Africa yashinikiza wanawake Kujituma kiajira

Maafisa wa kutetea haki za binadam hapa Pwani wametoa changamoto kwa wanawake kujituma zaidi upande wa ajira ili kujitegemea tofauti na kutegemea wanaume.

Wakigusia visa vya mauaji ya wanawake ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa hapa nchini, afisa wa kutetea haki za wanawake katika shirika la Haki africa Salma Hemed, alisema visa vingi vinachangiwa na wanawake kukosa kipato na kuishia kutafuta wanaume kwa ajili ya kipato cha haraka.

Akizungumza na sauti ya pwani Ijumaa tarehe 9 mwezi februari Salma aliongeza kuwa wanawake wangi huhatarisha maisha yao katika harakati hizo za kutafuta pesa kutoka wanaume.

Salma aidha alidai swala la wanawake kuwezeshwa kwa kiwango kikubwa na kuachwa nje mtoto wa kiume lilipelekea ongezeko la dhulma za kijinsia ikiwepo visa vya mauaji hasa yanayolenga jinsia hiyo.

“kama shirika tumekuwa tukifanya utafiti wa chanzo cha mauaji ya kiholela ya wanawake na tumeoona sababu tofauti ambazo zimeendeleza mauaji kama hayo,sababu kuu ni hali ngumu ya uchumi na kutokana na mila na desturi zetu wanawake wanategemea wanaume.” Alisema Salma.

Vilevile alisema kuwa serikali inapaswa kuwatengea wanawake ajira ambazo zinawezafanyika bila ya vigezo vingi kama vile ususi, kuchorwa piko na upambaji ili waweze kujitegemea na kupunguza visa vya mauwaji kwa wanawake.

“Jambo lengine ni kwamba serikali inapaswa kutoa usaidizi wa kifedha kwa kila kaunti kwa wanawake atakama ni kwa mkopo ili kuanzisha na kujiendeleza kibiashara na vilevile serikali iwape mafunzo ikiwa fedha izi zitakuwa almradi waweze kujihimili na kuendesha biashara zao ili ziendelee na kustawi badala ya kufa”Aliongezea Salma.

BY NEWS DESK