HabariMakalaNews

Aliyekuwa Mkuu wa Polisi Pwani Aaga Dunia

Aliyekuwa msaidizi wa Inspekta jenerali wa polisi Zachary King’ori Mwangi amefariki mapema leo.

Mwangi amefariki katika hospitali moja jijini Nairobi alikokuwa akipokea matibabu.

Kulingana na taarifa ya familia yake Mwangi alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi na ameaga dunia kutokana na matatizo yanayohusiana na upasuaji wa matibabu aliyokuwa akipokea.

Mwangi aliwahi kuhudumu kama Mkuu wa Polisi Mkoani Pwani, Nairobi na Eneo la Magharibi mwa Kenya kabla ya kuteuliwa kuwa msaidizi wa Inspekta Jenerali wa polisi.

Aidha aliwahi kuhudumu katika wizara ya mambo ya nje kabla ya kustaafu mnamo mwaka 2020.

BY MJOMBA RASHID