HabariLifestyleMazingiraNewsUncategorized

Jamaa Mmoja Kilifi ahukumiwa Kifungo cha Miezi 2 Jela kwa Ulaghai

Mahakama ya Kilifi imemhukumu kifungo raia cha miezi 2 ‘civil jail’ mwanamume mmoja anayeshukiwa kumlaghai mwenzake shilingi milioni 5.4.

Christopher Karisa Kazungu anadaiwa kumlaghai Lenox Mwadoya Mwasirya mali ya kujengea ukuta yenye thamani ya shilingi milioni 3.6 mnamo Julai 5 mwaka 2018 eneo la Kilifi Township .

Hakimu mkuu wa mahakama hiyo Julius Nang’ea ametoa adhabu ya kifungo hicho baada ya mshukiwa Christopher Karisa Kazungu kukwepa vikao vya mahakama pamoja na kudinda kumlipa deni lake Lenox Mwadzoya Mwasirya.

Mahakama hiyo imepinga ombi lililowasilishwa na Olwande Oballa wakili wa mshtakiwa la kutaka kupewa muda wa mwezi mmoja ili mteja wake akamilishe deni hilo la shilingi 4.4 baada ya kulipa shilingi milioni 1 kwa mlalalmishi.

Hata hivyo wakili wa mlalamishi Elisha Komora Dullu alielezea mahakama kuwa mshukiwa amekuwa akikwepa vikao vya mahakama tangu alipoachiliwa kwa dhamana hali anayodai kuwa inamnyima haki mteja wake.

BY ERICKSON KADZEHA