HabariMakalaMombasaNews

Miili 429 ya Shakahola Kuzikwa katika Kaburi la Pamoja

Huenda miili iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi ikazikwa katika kaburi la pamoja, Haya ni kwa mujibu wa Mwanapathalojia mkuu wa serikali Johanssen Oduor.

Akizungumza katika kongamano la afya la taasisi ya kimatibabu ya KEMRI jijini Nairobi, Oduor alieleza kuwa baadhi ya miili hiyo imeharibika pakubwa na kuwapa changamoto pale walipotaka kuitambua.

Kulingana na Oduor hatua ya baadhi ya watu kutoka familia zilizopoteza wapendwa wao kukataa kuenda kufanyiwa vipimo vya DNA ili kulinganisha vipimo hivyo na vile vya miili iliyofukuliwa ni miongoni mwa sababu zilizochangia uamuzi wa huo.

Kufikia sasa jumla ya miili 429 imefanyiwa upasuaji huku matokeo yake ya DNA yakiendelea kusubiriwa.

Mwisho