HabariLifestyleNews

Mashirika ya Haki Yaibua Wasiwasi kuhusu Tofauti za EACC na ODPP Katika Vita dhidi ya Ufisadi

Mashirika ya kutetea haki za kibinadam nchini sasa yameibua wasiwasi kuhusu tofauti za kikazi kati ya Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi, EACC na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) katika via dhidi ya ufisadi.

Katika taarifa ya pamoja mnamo Jumapili, Tume ya Haki za Binadamu Nchini KHRC na Shirika la Kimataifa la Transparency International (TI-Kenya) zilisema Ofisi hizo mbili zimeonesha tofauti na kuhitilafiana katika Kubaini hatima ya kesi za ufisadi suala ambalo linatishia uadilifu wa kupambana na ufisadi nchini.

Wakipigia mfano kesi kadhaa, mashirika hayo yalitaja kesi ambapo Ofisi ya DPP inapania kuwaondolewa mashtaka Maofisa watatu wakuu Serikalini wa Kampuni ya Kawi ya Geothermal Development kwa kile ODPP inasema ni ukosefu wa ushahidi wa kutosha lakini EACC ikipinga hilo na kusema kuondolewa kwa kesi hiyo kunaweza kuendeleza matumizi mabaya ya michakato ya kisheria.

“Mzozo sawia uliibuka Februari 16 2024, kuhusu kuondolewa kwa mashtaka dhidi ya waliokuwa Wasimamizi wa Mamlaka ya Kenya Pipeline, na hivyo kuthibitisha ukosefu wa maelewano kati ya EACC na ODPP katika kufuatilia kesi za ufisadi,” ilisema taarifa hiyo.

Mashirika hayo aidha yameibua wasiwasi kuhusu kuondolewa kwa kesi zinazohusisha watu mashuhuri ambao wanaaminika na ODPP kuwa na uhusiano mkubwa wa kisiasa na wakuu serikalini, suala ambalo limepelekea ubadhirifu wa hazina ya fedha za umma.

Kutokana na hayo sasa mashirika hayo yemependekeza kwamba Tume ya EACC inapaswa kupewa mamlaka ya kuendehsa mashtaka na kesi moja kwa moja.

Wakati huo huo wamependekeza kuwa waendesha mashtaka wanapaswa kuwajibishwa vilivyo kwa usimamizi mbaya wa kesi ili kukabiliana na suala la mapuuza ya wajibu na jukumu la uendedhaji mashtka.

BY MJOMBA RASHID