HabariLifestyleNews

Ruweida Obo: Wapeni Machifu wa Lamu Silaha Kukabiliana na Walanguzi

Serikali imetakiwa kuwakabidhi machifu wa kaunti ya Lamu silaha ili kuimarisha vilivyo vita dhidi ya mihadarati.

Mbunge wa Lamu Mashariki Capt. Ruweida Obo amesema kutokana na vitisho wanavyopokea machifu kutoka kwa walanguzi wa mihadarati ipo haja machifu wa kaunti hiyo hasa eneo la Lamu mashariki kukabidhiwa silaha hizo kama tahadhari.

Akizungumza katika Kongamano la Kupambana na Pombe haramu na dawa za kulevya eneo la ASK Mkomani mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Ruweida alisema tayari machifu watatu wamepoteza maisha yao katika harakati za kupambana na ulanguzi wa mihadarati eneo hilo huku wengine wakitishiwa maisha.

“…Wapeni Machifu silaha, maanake mnajua mimi kule kwangu machifu watatu wameuawa kwa sababu ya mambo ya mihadarati. Iko kwenye rekodi machifu watatu wameuawa,” alisema.

Wakati uo huo Ruweida alinyoshea kidole cha lawama Idara ya usalama ya kaunti ya Lamu kwa kuzembea katika kupigana na janga hilo la mihadarati.

“Tafadhali msituletee maafisa ambao ni adhabu mkawaleta kule kwetu ambao hawana cha kupoteza wanaachia watu w akule dawa za kulevya.

Ruweida aidha alirai kuongezwa maafisa wanawake zaidi kukabiliana na tatizo la mihadarati.

Kule watu wakifanyiwa msako wanawake wanakataa kushikwa

BY MJOMBA RASHID