BurudaniEntertainment

Tik tok yazindua programu mpya

Mtandao wa kijamii wenye umaarufu ulimwenguni Tik tok umezindua programu mpya ya Add to Music App kwenye mataifa mapya 163 nyakiwemo mataifa 41 yanayopatikana afrika kwenye ukingo wa sub-sahara.

Programu hiyo ya Add to Music App huboresha nguvu ya ugunduzi wa muziki kwenye TikTok ili kuendesha moja kwa moja utumiaji wa muziki kwenye huduma kuu za utiririshaji muziki.

Kutokana na mafanikio ya uzinduzi mwaka 2023, hivi majuzi mtandao huo ulitangaza kuwa programu hiyo ya Add to Music App itawafikia watumizi katika mataifa hayo ikiwapo taifa la Kenya na Nigeria.

App hii inawapa fursa wapenzi wa mziki kuhifadhi nyimbo wanazozigundua kwanye Tik tok, hasa katika huduma za utiririshaji wanazopendelea kwa kuzingatia upatikanaji wake.

Add to Music App imeboreshwa kusaidia mashabiki wa mziki kupata nyimbo wanazozipenda katika mtandao huo.

Huduma hii hujitokeza kama kinachoashiria Add Song, karibu na jina la wimbo, chini ya video ya Tik Tok kwenye ukingo wa For You Feed, na hukaribisha watumiaji kuhifadhi nyimbo hizo vile vile.

BY JOSEPH JIRA