HabariNews

Mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa mashamba umeagishiria hatua kuu humu nchini.

Haya ni kulingana na msimamizi wa mazingira na ardhi pamoja na mali asili Husna Mbarak

Akizungumza na Sauti ya Pwani fm Husan amesema kuwa kuna miradi tofauti tofauti inayoshirikiana na nchi za Uingireza inayohimiza mfumo  wa kidijitali hususan katika umiliki wa ardhi hapa nchini na nchi za nje.

Vilevile amesema kuwa miradi hii imewekwa ili kuhakikisha mipangilio kama vile usimamizi wa ardhi uko sawa.

“Mradi huu unanahkikisha teknolojia inatumika kwa njia zote, kwa njia ya upangaji,usimamizi,umiliki ,tunasema deta na kila kitu kuhusiana na hio ardhi zinaekwa kwa njia ya kidijitali zaidi ya hapo ni kuhakikisha kumewekwa mipangilio ya kuhakikisha ile ardhi imeweza kutumika kwa njia inayostahili.” Alisema Husna.

Kando na hayo msimamizi huyu amesema kuwa tayari gatuzi mbili za Tanariver na Kilifi katika ukanda wa Pwani zimeanza kuunga mkono mfumo huu bila kusahau kaunti ya Kwale, Lamu na Taita Taveta ambazo zimeweza kuunga mkono mfumo huu kikamilifu.

Vile vile Husna ameongeza kuwa vifaa vya kidijitali vimefika katika kaunti hizi na ni jukumu lao kama wataalamu kuwafundisha taaluma ya jinsi ya kuvitumia.

“umuhimu ni kuhakikisha kuwa ile mipangilio imewekwa na ile mizozo kuhusiana na mipaka imeweza kutatuliwa,tayari kunazo kaunti katika hili jimbo la Pwani wameweza kuhakikisha wameunga mkono lakini huu mradi unaendelea kuwaunga mkono na wengine pia kuanza kutumia huo mfumo.” Alisema Husna.

BY EDITORIAL