HabariNews

Wanawake Wahimizwa Kujiunga Na Vikundi

Kina mama wamehimizwa kujiunga na vikundi mbali mbali ili kuweza kufaidika na fedha za serikali katika juhudi za kujiendeleza na kutengeneza nafasi za ajira.

Akizungumza kwenye kikao na kina mama wa chama cha UDA eneo la Mtopanga mshauri wa rais katika maswala ya siasa Karisa Nzai alisema serikali imetenga fedha za vikundi vya kina mama akidokeza kuwa tayari amefanya mazungumzo na waziri wa Vyama vya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo Simon Kiprono Chelugui kuhusiana na swala hilo.

Vile vile Nzai aliongeza kuwa ukosefu wa ufahamu kuhusu mikakati ya kuchukua mikopo imelemaza maendeleo ya vikundi mbali mbali ambavyo huchipuka wakati wa siasa na kufifia siasa zinapoisha.

“Nafasi za kina mama kuwa zipo sasa serikali iko na pesa lakini zile pesa zinakuja kama mmejiunga kikundi mimi nilishazungumza na waziri lakini shida ni   walikuwa hawajafundishwa kuhusu kukopa pesa,vikundi vimekuwa vingi siasa ikifika wanapewa pesa wanakula wanaanguka,sasa nataka hivi vikundi vijiunge haraka” Alisema Nzai

Wakati huo huo Nzai aliwataka viongozi walio mamlakani kufika sehemu za mashinani na kueleza umma kwa nini hawajatimiza ahadi walizoweka wakati wa kampeni za siasa, licha ya wananchi kuwa na matumaini makubwa.

“Ni haki yenu na wakaazi na wapiga kura kuwa na matarajio ambayo hayajafanyika na kweli ni lazima kuwe na kutofahamu lakini pia ni jukumu la viongozi kurudi chini mashinani pia kueleza waanchi kinachoendelea,wajua kama kule juu wafungiwa si urudi uje uwaambie nafungiwa ndio muelewe.” Alisema Nzai

Kuhusu swala la ajira Nzai aliweka wazi kuwa serikali imatenga nafasi zaajira zinazopatikana katika mamlaka ya kitaifa ya ajira.

“Kama kunao wasichana ambao wamesomea kazi ya uuguzi wako na kazi tutapeleka Saudi Arabia watajiendeleza,sasa mtu akisema nafasi za kazi serikali haina ni kwa sababu ilikuwa hakuna namna ya kuunganishwa hizo kazi,serikali iko na nafasi za kazi sai 8,500,ziko kwenye mamlaka ya kitaifa ya ajira huko huna haja ya kumjua gavana,mbunge wala mtu yeyote.” Alisema Nzai.

BY MEDZA MDOE