HabariNews

Gavana Mung’aro asaini mkataba na SHOFCO

Gavana wa kaunti ya kilifi Gideon Mung’aro amesaini mkataba wa maelewano na shirika la kijamii la shining hope for urban communities SHOFCO.

Mkataba huo utawezesha serkali ya kaunti na shirika hilo kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ya jamii katika sekta za elimu, kilimo, maji, afya na masuala ya kijinsia.

Akizungumza katika hafla hiyo Mung’aro amelipongeza shirika hilo akisema serkali yake iko tayari kujenga jumba la maonyesho kwa ajili ya wakaazi watakaokuwa katika shirika hilo.

“Leo tumesaini mkataba huu ili tuweze kuwa na mikakati ya maendeleo ya vijana na kina mama na tutakuwa na mwelekeo,nataka tujenge bohari ambapo vijana wetu ambao wametoka katika vyuo vya kiufundi wataweza kutengeneza bidhaa zao na kuwe na jumba la maonyesho.” Alisema Mungaro

Kwa upande wake mwanzilishi na Mwenyekiti wa shirika hilo Dkt Kennedy Odede amesema shirika hilo litashirikiana na serkali ya kaunti kuhakikisha miradi yake inafanikiwa ukiwamo ule wa kujenga jumba la maonyesha ya bidhaa mbalimbali.

“Shikeni Mkono gavana wenu vizuri sisi tuko na mpango wa kushirikiana ili kuhakikishe miradi ya maendeleo inatimia katika kaunti hii na tumeona eneo hili .” Alisema Odede

Katika ziara hiyo kwenye Odede pia amezindua rasmi jengo la ghorofa tatu na kisima cha maji ili kuwanufaisha wakaazi wa eneo la kiwandani na kilifi kwa ujumla.

BY EDITORIAL DESK