HabariLifestyleNews

Maandamano; Walimu wa Sekondari Msingi (JSS) Wasusia kazi Wakishinikiza Serikali Ishughulikie Matakwa yao

NA huku shule zikifunguliwa rasmi kwa muhula wa 2 Jumatatu Mei 13, Walimu wa Shule za Sekondari ya msingi (JSS) kaunti ya Mombasa wameanza mgomo wao rasmi.

Walimu hao wamesusia kazi wakiweka bayana tishio lao kwa kufanya maandamano kuishinikiza Tume ya kuajiri Walimu nchini, TSC kuheshimu na kutekeleza matakwa yao mara moja.

Wakizungumza na waandishi wa habari hapa mjini Mombasa walimu hao wamekashifu tume hiyo kwa kuhujumu makubalano yao ya awali kuwa ingewapa kandarasi ya kudumu ifikiapo Desemba 23 mwaka 2023.

Kulingana nao, TSC sasa inawataka watie sahihi kandarasi nyingine fupi badala ya kuwapa muktaba wa kudumu.

“TSC isituruke ikidai haitujui na wao ndio waajiri wetu walitupa mkataba wa muda wakatuka nambari ya uajiri ya TSC, ni sababu gani walituambia tutiea saini Mkataba Janauri 2023 na kutuambia ikifika Disemba 23 watatupa mkataba wa kudumu.” Alisema Obara Kelvin Kaimu Mwenyekiti wa Muungano waw a walimu JSS, Mombasa.

“Ni sehemu gani ya mkataba, sehemu gani ya katiba inasema tunapaswa kuwa mkataba wa walimu wanagenzi wa miaka 2?” Aliuliza mmoja wa walimu hao.

Walimu hao aidha wamelalamikia mshahara wa shilling elfu kumi na saba wanaolipwa kwa mwezi wakisema mshahara huo hautoshi kukidhi mahitaji yao.

Kwa mujibu wao,mshahara huo ni kidogo na baadhi wamelazimika kuchukua mkopo ya madeni hali ambayo imelemaza na kuwafanya kutomudu gharama ya maisha.

NA HUKO kaunti ya Nakuru ZAIDI ya walimu 2000 wameshiriki wakidai hawatorejea darasani matakwa yao yatakapoangaziwa na tume ya kuajiri.

Vile vile walimu hao wanasema serikali inafaa kuwalipa ili kuhakikisha wanafanikisha utekelezwaji wa mfumo mpya wa elimu ya umilisi CBC.

Walimu hao wametoa wito kwa serikali kupitia TSC kusikiliza kilio chao la sivyo mgomo huo utaendelea hadi pale matakwa yao yakatekelezwa kikamilifu.