HabariNews

Athari Za Upepo Mkali Unaotokana Na Kimbunga Ialy

Athari za upepo mkali  unaotokana na kimbunga Ialy zimeendelea kushuhudiwa katika ukanda wa pwani takriban watu wawili wakipoteza maisha na kuwaacha wengine 6 na majeraha katika kaunti ya Kilifi.

Kulingana na taarifa ya polisi ni kwamba mmoja kati ya wawili hao walioaga dunia ni mtoto wa shule wa miaka 4.

Katika kaunt ya Mombasa Kimbunga hicho kimesababisha mmiliki mmoja wa mgahawa kupoteza mali zake baada ya mti kuangukia mgahawa huo.

Akizungumza na Sauti ya pwani Joseph Maselo mmiliki wa mgahawa huo alieleza kwamba mti huo ulikuwa na ishara ya kuvunjika kabala ya upeo huo na kuanza kuchukuwa tahadhari.

Maselo alibainisha kuwa aliwasiliana na idara ya usimamizi wa misitu kaunti ya Momabasa kuangalia hali ya mti huo ila juhudi zake haziku za matunda kwani maafisa hao walifika wakati mti huo umeagushwa na upepo huo.

Hata hivyo aliongeza kuwa hakuna waliojeruhiwa katika mkasa huo kwani tayari wateja wake walikuwa amewaagiza kukaa nje kwa usalama wao.

“So mimi ikianguka tulijua kwamba itaanguka, kwa sababu upepo wa leo ulikuwa kali sana. Vile crack ililia tukajua leo tuko katika hatari,” alisema Maselo.

Kulingana na idara ya utabiri wa hali ya anga nchini Kimbunga Ialy kinatarajiwa kuendelea wiki hii.

Maselo sasa ansema hajui ataanzia wapi baada ya mkasa huo ambao umesababisha hasara katika bishara yake.

“So kazi yetu imesimama hatujui tutaanzia wapi,na kama kaunti yenyewe hatujui itatusaidia vipi kwa sababu kila leseni wakitaka…hata wafanyikazi wangu sijui wataenda wapi, hata sijui itakuwaje.” Aliongeza Maselo.

BY NEWS DESK