HabariNews

Jamii yahimzwa kukumbatia malezi ya zamani

Viongozi wanawake kaunti ya Mombasa wameeleza haja kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao wakati huu ambapo maisha yamekuwa magumu na utovu wa maadili kuongezeka.

Kiongozi wa maenedeleo ya wanawake Wadi Ya Shanzu mjini Mombasa Joyce Awuor alisema kwamba baadhi ya wazazi wamekuwa chanzo cha watoto kupotoka kimaadili, kushuhudiwa kwa mimba na ndoa za utotoni.

Akizungumza na Sauti ya Pwani siku ya Jumatano Mei 22 mwaka huu, alidai kuwa wazazi hawafuatilii watoto wao hali iliyopelekea kupatana na marafiki ambao hawafai.

“Unakuta mtoto msichana anawachwa anapewa freedom.Mzazi awe mwangalifu ajue mtoto anatembea na watu gani, akiingia anatoka sangapi na anarudi sangapi na ile company ambayo anatembea nayo,” Alisisitiza Awuor.

Kauli ya Awuor ilipigwa jeki na baadhi ya wazazi mjin ambao walidai kuwa ni asilimia ndogo ya wazazi ambao wamezembea katika malezi ya kimaadili.

Kulingana na wazazi hao kunaumuhimu wa kukumbatiwa kwa malezi ya miaka ya awali malezi na kumrekebisha mtoto lilikuwa ni jukumu la jamii wala sio la mzazi pekee.

“Tujaribu kama maisha ya zamani vile tulikuwa tunashughulika na mtoto akiwa amekosea, unamwambia wewe wafanya nini hapa, kidogo wamkemea, lakini siku hizi sasa jaribu, thubutu ndugu yangu uone,” alisema mmoja wa wazazi hao.

Ili kukabiliana na chanagmoto mbalimbali ibuka zinazowakumba watoto hasa wa jinsi ya kike, Awuor alisisitiza umuhimuwa kubuniwa mikakati mwafaka.

Kulinga naye kuzinduliwa rasmi kwa mafunzo ya ukuaji katika ngazi mbalimbali ya mtoto kwenye shule zote nchini kama vile suala la Kuvunja ungo, ngono na athari zake itasaidia pakubwa kuokoa kizazi cha sasa na hata vizazi vya baadaye.

BY EDITORIAL DESK