HabariNews

Wito Umtolewa Kwa Jamii Kuunga Mkono Kina Mama Wajane Na Vijana Walioasi Uhalifu

Wito umetolewa kwa jamii kuunga mkono kina mama wajane na vijana walioasi uhalifu na magenge ili waweze kujiendeleza na kukimu mahitaji yao.

Katika mahojiano na Sauti Ya Pwani, wajane hao waliojiunga kwa kundi moja la Likoni Widows Women Group, chini ya mwenyekiti wao Khadija Yusuf eneo bunge la Likoni, ameeleza kuwa kina mama wajane hupata changomoto nyingi pindi bwana zao wanapofariki jambo ambalo huwalazimu kuombaomba ili kukidhi mahitaji yao yakiwemo ulezi na mahitaji ya watoto yatima walioachwa nyuma.

Hata hivyo, Khadija na wenzake 36 wamedhihirisha kuwa wanaweza kujitoa katika matatizo hayo kwa kuungana na kuanzisha miradi inayowasaidia kupata kipato, ikiwemo biashara ya kuoka keki, donasi na mikati pamoja na biashara ya kutengeza sabuni za maji japo wakiwa na changamoto za vifaa na mahitaji mengine ya biashara hiyo.

Mashine ya kuoka(oven) inayotumia makaa

Kwa upande mwengine, vijana mablimbali kutoka eno la Likoni nao wameamua kuondoa dhana ya kuwa vijana wasiokuwa na kazi ni wahalifu, kwa kuungana na kusajili kikundi kwa jina AL- RAZAQ furniture group wakiwa vijana 26 ambao wanatumia talanta yao ya kutengeza samani kama makochi, viti, vitanda na makabati ilikujikimu kimaisha na kuepuka makundi ya uhalifu.

Kundi la vijana la Al-Razzaq wakitengeneza bidhaa za mbao kwenye banda lao eneo la Likoni

Vijana hao na kina mama wajane wameomba viongozi na wafadhili kujitokeza na kuendelea kuwaunga mkono kwa kuwasaidia kupata ujuzi zaidi wa kuboresha bidhaa zao ili kupata soko kubwa zaidi baada ya ofisi ya mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa kuisikiza kilio chao na kuahidi kuwapa usaidizi ili kuoboresha bidhaa zao na hata kufaidika na mfuko wa NGAAF.

BY SOPHIA ABDHI