HabariNews

Wasiwasi wagubika sekta ya ajira washikadau wakionya dhidi ya ongezeko la Wafanyakazi wanaougua Maradhi ya Akili

Wizara ya utoaji huduma za serikali imeeleza wasiwasi wake kuhusiana na ongezeko la wafanyakazi wanaokabiliwa na maradhi ya Akili.

Katibu katika idara hiyo Amos Njoroge Gathecha alionya kwamba ongezeko hilo linaashiria changamoto mbalimbali ambazo wafanyakazi wanapiti katika maisha yao wakati wanapoendelea kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Akizungumza katika warsha ya wakurugenzii wa masuala ya wafanyakazi mjini Mombasa, Gathecha aliwaagiza wakurugenzi hao kufuatailia kwa karibu dalili za maradhi ya akili mapema kuhakikisha utendakazi wa wafanyikazi wao unaimarika.

“Katika mwaka 2020/2021 tuliona wafanyanyikazi wa uma 13,000 ambao walikuwa na changamoto za kiakili, Tunatarajia idadi hiyo kuongezeka kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Juni, tutapata takwimu kufikia mwisho wa huu mwaka huu wa kifedha.

Kwa hivyo haya masuala ni kihalisia na ni wakati wa kuchukuwa muda kushughulikia suala hilo kwa uangalifu mkubwa,” alisema Gathecha.

Kwa upande wao wataalamu wa akili wakiongozwa na Dakt.Vincent Hongo kutoka hospitali ya Chiromo walieleza haja kwa maradhi ya akili kujadiliwa kwa uwazi ili kukabiliana na unyanyapaa.

Alisisitiza kwamba endapo hatua mwafaka hazitachukuliwa kukabiliana na tatizo hilo katika sehemu za kazi, huenda athari ikawa mbaya zaidi.

Ni lazima kuwe na mabadiliko ya kimtazaamo. Njia ambazo tunatumia tunaangazia afya ya akili na afya njema katika maeneo ya kazi.

Leo tunawalika wakati tunapopanua uhusiano wetu kwamba tunafaa kubadilisha na kwa kiasi kikubw turekurekebish jinsi tunavyoangazia afya njema kama wasimamizi.

Sisi sio robot, sisi sio mashine, lazima tufanye kile tunachotakiwa kufanya kwa sababu tusipofanya, usimamizi wetu utaathirika” alieleza Dakt. Hongo.

 

Pia unaweza kusoma;

https://sautiyapwanifm.com/2024/05/28/serikali-yatakiwa-kuwekeza-kwenye-sekta-ya-afya-kukabiliana-na-ongezeko-la-matatizo-ya-afya-ya-kiakili/

 

BY MAHMOOD MWANDUKA.