HabariNews

Mwenyekiti wa hazina ya vijana Fatma Barayan aeleza haja ya kuwezeshwa kwa wanawake kibishara

Mwenyekiti wa hazina ya kitaifa a Vijana Fatma Barayan ameeleza haja ya kina mama kujumuishwa katika harakati za maendeleo hapa nchini.

Akizungumza katika wakati wa kongamano la hamasa kwa wanachama wa UDA kuelekea uchaguzi wa mashinani wa chama hicho baadaye mwezi huu, Barayan alisema kwamba kina mama wana jukumu kubwa kufanikisha maendeleo.

Kulingana na Mwenyekiti huyo, kuwezeshwa kwa kina mama kwenye masuala ya ajira na mafunzo kuhusu ufanisi wa kibiashara kutasaidia kufanya mageuzi na kujihakikishai uhuru wa kiuchumi kwa kujinasua kutokana na umaskini.

“Nataka kuwaambia kwamba there is no freedom without financial freedom. Na ndio maana kama kina mama kuendeleza bishara zetu katika jamii, ili kuendeleza mchango wetu katika Uchumi wa jamii, lazima tupate mafunzo ya kibishara. Lazima tueleze kusomeshwa na ni njia gani tutakuza bishara na kutafuta ajira kwa jamii zetu hapa.” Alieleza Barayan.

Wakati uo huo Barayan alisisitiza umuhimu wa wanachama na viongozi wanaopania kuwania nyadhfa mbalimbali katika uchaguzi huo kushirikiana kwa manufaa ya wanachi na chama cha UDA.

Akiwahimiza wanachama kujitokeza kupiga kura, Barayani ambaye anawania kiti cha mwakilishiwa wa wanawake kaunti ya Mombasa katika uchaguzi huo wa mashinani Aliwataka wanachama wa chama hicho kumchagua katika wadhafa huo.

Aliahidi kuwa mstari wa mbele kutetea na kupigania masuala ya kina mama na vijana katika kaunti ya Mombasa.

“Tumeweza kuwaita nyote Mombasa wale viongozi 4,5 60 na sis tumejipanga, hili ndilo jeshi la Hassan Omar Hassan 2027, hili ndio jeshi la Fatma Barayan 2027 hili ndio jeshi la viongozi wote watakaogombania nyadhfa wanaopigania viti tofauti katika UDA 2027.

Na mimi langu ni kuwahamasisha na kuwasihi kwamba tarehe 22 tujitokeza kwa wingi tuweze kupata hizi viti, lazima tupendane na tushirikiane…” Aliongeza Barayan.

BY MAHMOOD MWANDUKA