HabariNews

Bado Sana! Rais na Naibu Wake Wapata Alama ya D kwenye Kura ya Maoni kuhusu Utendakazi

Utafiti wa Kura ya maoni ya Infotrack kuhusu utendakazi imewapa Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua alama ya D.

Rais na naibu wake wamepata alama hiyo ya kwa asilimia 46 katika utendakazi ulioangazia masuala mbalimbali serikalini.

Kwa mujibu wa kura hizo Wakenya wameonyesha kuridhishwa na utendakazi wa Waziri wa mambo ya ndani Prof. Kithure Kindiki ambaye amepata alama ya B ya aslimia 60, naye waziri wa Michezo Ababu Namwamba akifuatia kwa asilimia 51.

Mtafiti Mkuu wa Infotrack amesema kulingana na kura hizo Waziri aliyefanya vibaya ni Waziri wa Kilimo Mithika Linturi aliyeshika nafasi ya mwisho kwa alama ya E akifuatwa na waziri wa kawi Davis Chirchir

Utafiti huo wa Infotrack aidha uliweka utendakazi wa Upinzani, Bunge na idara ya mahakama kwa alama ya D huku kwa jumla utendakazi wa Baraza la mawaziri ukitajwa kuwa chini kwa alama ya D.

Kura hiyo ya maoni ilifanywa kati ya tarehe 23 na 26 mwezi Mei mwaka huu huku watu 1,700 wakihojiwa.