HabariLifestyleMazingiraNews

JAMII YAHIMIZWA KUTUNZA MAZINGIRA YA FUO ZA BAHARI ILI KUPUNGUZA HATARI ZA UCHAFUZI WA MAZINGIRA YA FUO ZA BAHARI

Huku maatdhimisho ya siku ya kimataifa ya bahari yakitia kikomo jamii imehamasishwa kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari ilikupunguza hatari zinazotokana na uchafuzi haswa ule wa taka za plaskini katika tamasha la siku tatu lililoandaliwa eneo la word of life Diani, kaunti ya kwale.

Wadau tofauti walioshiriki katika katika kilele cha tamasha kubwa la zero plastic festival lililoandaliwa na shirika la samabasports youths agenda, walipata fursa yakuhamasisha jamii kupitia hotuba na hata michezo

Afisa wa huduma za kwanza kutoka community 911 akitoa huduma Kwa mchezaji wa handball

“baada ya siku tatu za tamasha hilo , tumekusanya takriban tani 7 za taka za plaski zaidi ya malengo yetu ya tani tatu tulizotarajia kukusanya japo pia kuna changamoto ya aina mpya ya taka zinazotokana na vifaa vya electroniki maarufu kama e -waste na tutashirikiana na washikadau kuunda kamati ya kulitatua hilo siku za usoni” asema mkurugenzi wa shirika la samaba sports youth agenda , mohammed Mwachausa.

Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa shirika la udhibiti wa shughuli za mazingira nema kaunti yak wale Dancan Okoth ameeleza kwa licha ya kuwepo kwa sheria kali za kudhibiti mazingirakuna utepetevu katika idara ya mahakama katika kutoa hukumu kwa wanaoshtakiwa, na pia hatari inayowakodolea maafisa wa nema wanapokwenda kuwatia mbaroni wanaovunja kanuni hizo.

Baadhi ya washikadau waliofanikisha tamasha hilo

“kuna changamoto haswa katika idara ya mahakama kwani faini iliyowekwa na NEMA hufika hata milioni 4 lakini mahakama wakati mwengine hushindwa kuendeleza kesi hizo, pili, mipaka yetu iko wazi mno haswa kwa kanuni za ujirani kwani kenya imepiga marufuku baadhi ya plastiki lakini Jirani zetu Tanzania hawajafanya hivyo na tatu swala la usalama pia ni changamoto haswa tunapokwenda kushika mtu aliyevunja sheria za mazingira, tunawezwa hata kupigwa kama hatuna usaidizi wa polisi” akiongeza Okoth

Vijana nao wametakiwa kujiunga m,afunzo ya vyuo vikuu kusomea taaluma zinazohusiana na mwaala ya bahari na mazingira ya uchumi samawati ilikuonyakua nafasi za ajira zinazotokea na kufaidika na maswala ya uchumi samawati na