HabariNews

KISHRA yaitaka SRC Kubadili Sheria Ya Kupunguza Marupurupu

Muungano wa hoteli na migahawa eneo la Mtwapa kaunti ya kilifi KISHRA wameitaka tume ya kusimamia mishahara na marupurupu ya wafanyakazi SRC kujadili upya sheria ya kupunguzwa kwa marupurupu ya wafanyakazi wa serikalini

Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano huo Michael Mwiha ambaye pia ni mkurugenzi wa Mtwapa Country Resort, wamedai kuwa huenda baadhi ya hoteli zilizoko eneo la Mtwapa zikalazimika kufunga kabisa kutokana na kulemaa kwa biashara hali ambayo imepelekea wawekezaji wa hoteli hizo kuathirika pakubwa.

Michael Mwiha(katikati), Mwenyekiti KISHRA

Mwiha ameongeza kwa kusema kuwa, baadhi ya hoteli zimelazimika kuwafuta kazi wafanyakazi wao kutokana na kushindwa kuwalipa mishara yao kama walivyokuwa wakifanya hapo awali suala ambalo litachangia ukosefu wa ajira kwa wengi.

Kwa upande wake Yvonne Ayako  ambae ni katibu wa muungano huo na msimamizi wa hoteli ya Mawenzi amedai kuwa licha ya kuwasilisha barua kwa serikali ya kaunti na wizara ya utalii, hadi kufikia sasa hakuna msaada wowote uliotoka kutoka kwao.

Yvonne Ayako, Katibu wa KISHRA

Hata hivyo ametaka kuwasilishwe hoja bungeni ili sheria hiyo ijadiliwe upya kwani huenda ikaleta athari kubwa zaidi kwa hoteli zote zilizoko eneo la Mtwapa.

 

BY KHADIJA BINTI MZEE