Shirika la mawakala wa usafiri nchini kenya (KATA) lililalamikia ongezeko la ushuru na mabadiliko ya sera kama mojawapo ya changamoto ambazo zinatishia kulemaza sekta ya usafiri na shughuli nyinginezo ndani ya shirika hilo.
Katika mkutano wao kila mwaka ulioandaliwa hapa mjini Mombasa siku ya ijumaa 7 mwaka huu, viongozi wa shirika wakiongozwa na afisa mkuu mtendaji wa KATA Nicanor Sabula, kwa kauli moja walihofia kutatizika zaidi kwa shughuli za usafiri katika shirika hilo wakisema ongezeko la ushuru ni pigo kubwa kwa sekta hiyo ya usafiri.
“Kama biashara nyingine zile zote tuna ugumu kidogo na zile sheria ambazo za kichumi ambazo serikali inaanzisha hizi sheria haswa kwenye kipengele cha kodi kwa sababu ukiongeza ushuru kidogo ile hali ya kufanya biashara inakuwa vigumu kwa sababu kila mtu ana uzito mkubwa wa kimapato, Sekta hii yetu ya usafiri wakati mwingi hupigwa na tisho wakati ambapo gharama ya kufanya biashara imeenda juu kwa sababu kitu cha kwanza ambacho makampuni wataweza kufanya ni kusema wacha tupunguze usafiri,’’ alisema Nicanor Sabula.
Aidha viongozi walipendekeza kutekelezwa kikamilifu kwa sera zilizoko ili kupanua biashara ya utalii nchini wakisema hali ya angatua za ndege, mikahawa ya kitalii haijaafikia viwango vya kimataifa na sasa wanapendekeza kuboreshwa kwa sekta hizo hili kuwa kivutio kwa watalii.
“Unajua jambo hili la kupanua uchumi ya utalii sio kitu ya siku moja lakini ni kuangalia kuna malengo inayofaa kupanua hii biashara na tukiamgalia kwa vile miundombinu tuangalie kama ni uwanja wa ndege ama tuanglieni barabara.Pengine hazijafikia kile kiwango lakini kunai le nia na jinsi ya kuenda kuzifanyia ziwe za kiwango cha kimataifa kwa hivyo tunafurahia na zile sera zinaendele kufanywa ile itatakana ni kasi ya kufanya haya mambo yaendelee kuwa ya juu ndipo mtuweze kuinua hii biashara yetu kwa haraka.Ndio sababu tunabishana na nchi zingine na hizo nchi pia zinajituma kwa hivyo lazima sisi tujitume ndipo tulete hawa watalii hapa nchini mara ya kwanza nay a haraka ndio tuweze kufaidika kwa hiyo biashara ya utalii.” alisema Kithitu
Viongozi hao sasa walitoa wito kwa serikali kuwapa washikadau wa sekta ya usafiri muda zaidi ili kuweka mikakati inayofaa kuboresha huduma za shirika hilo wakilalamikia mabadiliko ya sera na utozaji wa ushuru kama baadhi ya changamoto zinazolemaza juhudi ya kuafikia malengo yao.
“Kama utalii wetu utakuwa ghali zaidi itakuwa watu wana chaguo si hapa tu Afrika lakini kote duniani .wana chaguo la kuenga na wacha tusifanye utalii wetu ghaki na tusiufanye ugumu.tuimarishe toleo letu la uchumi.hoteli zetu tuzijenge barabara tujenge viwanja vyetu wa ndege na pia tupate wawekezaji ambao watatupa mali mpya ndiposa tuweze kukuza uchumi wetu na pia tuwekeze sana kwa utalii wa ndani kwa sababu hapo ndipo kiteka uchumi kikubwa katika nchi.” aliongeza Kithitu
Kauli ya viongozi inajiri huku Shirika la ndege la Kenya Airways likiweka rasmi mkataba wa maelewano (MOU) na Muungano wa Mawakala wa Usafiri wa Kenya kama moja wapo ya juhudi za pamoja za kuimarisha ushirikiano katika shughuli zao.
Ushirikiano huo, ukilenga kuongeza uwepo wa soko la kutoa huduma wa kitaifa na pia kuongeza ushindani ndani ya mazingira ya sekta hiyo na mashirika mengine ukanda wa afrika mashiriki.
“Ikija kwa (MOU) tumesema kuwa (KATA) ni mshirika wetu muhimu kwetu kwa sababu ni wao hutusaidia kufikia wateja wetu na ni nwao hutusaidia kukuza biashara yetu sasa tunataka kukaza huo uhusiano ambao tunao na tunakuja na (MOU) ambayo haitaimarisha tu huo uhusiano lakini pia itapeana taarifa zaidi kwa wateja na lengo kuu ni kutembea vizuri pamoja kukuza biashara ,kujishikilia na mauzo yetu na pia kusaidia kufanya ubora wa wasafiri wanaoingia na wanaotoka kenya.” alisema Kilavuka
BY EDDAH SITUMA