HabariNews

CIPK Yaishauri Serikali kuzingatia Utawala wa Haki na Kutowabagua Wakazi wa Lamu

Viongozi wa kidini kaunti ya Mombasa wameokosoa Serikali kwa kile wanachodai ni ubaguzi wa kutojali  huduma muhimu kwa wanannchi.

Katibu Mkuu wa Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini, CIPK, Balozi Sheikh Mohamed Dor amesema kuna ubaguzi wa hali ya juu kwa baadhi ya maeneo wakati wa kupata huduma muhimu

Kulingana na Sheikh Dor kuna visa vya wananchi kutoka maeneo ikiwemo Lamu ambapo wanahangaishwa kupata stakabadhi muhimu kama vile vitambulisho na Pasipoti.

Nimezungumza na viongozi wetu wa CIPK Lamu wananishtakia kuwa kuna watu wameomba na ku apply passport mwaka mzima sasa hawajapata passport zao, wengine Wakenya wakiomba wanapata pasipoti kwa wiki tatu, mwezi hivi, Lakini maeneo fulani ambao pia ni Wakenya wakiomba hawapati na ni haki yao, wanahangaishwa.” Alisema.

Dor aliyewahi kuhudumu kama Mbunge maalum aidha amesema suala hilo ni miongoni mwa masuala ambayo yanafaa kushughulikiwa ili kila Mkenya ajihisi huru na kujivunia taifa lake.

Kadhalika akiongeza  kuwa Kenya ni taifa ambalo limekumbwa na suala la uongozi mbaya hali iliyopelekea visa vya ufisadi, ukosefu wa uwazi na uwajibikaji serikalini, kutoheshimu idara ya Mahakama miongoni mwa mengine.

“Jambo linalofanya Serikali nyingi kufanikiwa ni uongozi mzuri yaani masuala ya good governance na utawala wa haki. Ni kiungo kikubwa sana baina ya anayetawala na anayetawaliwa na kuhakikisha katiba na sheri inafuatwa. Mwananchi ajione popote anapoishi anachukuliwa sawa pasi kubaguliwa ndio linaloleta uongozi mzuri.

Kingine suala la ufisadi linapaswa kuangaziwa ili kuwa na utawala mzuri.” Alisema.

Kulingana na kiongoiz huyo, endapo serikali inahitaji kutuliza joto la kisiasa kuibuka kwa na mavuguvugu ya kupinga Serikali, ni sharti masuala hayo yaangaziwe kwa kina na nia safi.

By Mjomba Rashid