Waziri wa Vyama vya Ushirika na Biashara Ndogondogo Wycliffe Oparanya sasa ametishia kuwachukuliwa hatua kali watu wote waliokwepa kulipa mkopo wa hazina ya serikali ya Husler Fund.
Katika mahojiano ya kipekee na runinga moja nchini Oparanya amesema Wizara yake imeweka mikakati kabambe ikiwemo ya kufuatilia mkopo huo kutumia nambari za vitambulisho kuwatambua wote waliodinda kulipa.
Kulingana na Waziri huyo, takribani shilingi milioni 12 zilichukuliwa kipindi cha Waziri mtangulizi wake Simon Chelugui na hazijalipwa kufikia sasa na hivyo serikali itafanya kila iwezalo kurejesha pesa hizo kwa hazina ya taifa.
Wakati uo huo Oparanya ametoa wito kwa wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu kuanzisha biashara kujikimu kimaisha badala ya kutegemea ajira ya kudumu kutoka kwa serikali akiahidi kuwa serikali kupitia wizara yake itawapa wafanyabiashara wa viashara ndogondogo mtaji wa shilingi elfu 50 kuanzisha biashara zao.
By Isaiah Muthengi