HabariNews

Gavana Timami amteua James Gichu kuwa Naibu Gavana wa Lamu

Gavana wa Lamu Issa Abdallah Timami amteua James Gichu kuwa Naibu Gavana wake; uteuzi huu ukijiri kufuatia kifo cha naibu wake Raphael Munyua mnamo Spetemba 6.

Uteuzi huo unajiri baada ya shinikizo kutoka kwa jamii mbalimbali za eneo hilo hasa maeneo ya Kisiwani Lamu Mashariki kumtaka Gavana huyo kumteua Naibu wake kutoka eneo hilo.

Kwa upande wa wanaharakati wa masuala ya kijamii na uongozi wamekuwa wakishinikiza kuhusishwa kikamilifu kwa jamii za eneo hilo katika kutoa maoni yao kwenye mchakato wa kumchagua naibu gavana.

Walimtaka Gavana huyo kutoa orodha ya wateule wake kisha wananchi kushirikishwa kutoa maoni yao wa wanayempendekez.

Gichu anachukua wadhfa huo wa Unaibu Gavana kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia kifo cha Raphael Munyua.

By Mjomba Rashid