HabariNews

Rais Ruto Avunja Rekodi ya Kiongozi Fisadi Zaidi wa Mwaka akishikilia nafasi ya Pili Duniani.

Rais William Ruto amevunja rekodi kwa kuteuliwa kuwa ‘Mtu Fisadi wa Mwaka’ na ripoti ya shiirika la Mradi wa Kuripoti Ufisadi na Uhalifu ulioapangwa ‘Organized Crime and Corruption Reporting Project’ (OCCRP).

Kulingana na matokeo ya uteuzi wa shirika hilo Rais wa zamani wa Syria aliyeondolewa mamlakani Bashar Al-Assad aliorodheshwa kama ‘Mtu Mfisadi Zaidi’ huku Rais Ruto akimfuatia kwa karibu katika nafasi ya pili.

Rais Ruto amepokea uteuzi wa zaidi ya 40,000 uliomweka nafasi hiyo ya pili aliyoshika rais Ruto inajiri huku shirika hilo la OCCRP likikiri kuwa uteuzi huo wake ni wa kihistoria hasa baada ya kupokea uteuzi mkubwa zaidi wa umma katika historia ya shirika hilo.

Kulingana na shirika hilo, Wakenya walimteua kwa wingi Rais Ruto katika kitengo hasa kutokana na masuala mbalimbali tata yaliyowakwaza ambayo yamedhoofisha utawala wake, haswa mwaka wa 2024.

Shirika hilo lilichukua maoni na uteuzi wa umma kwa kiteng hicho cha Mtu fisadi zaidi mnamo mwezi Novemba.

Wakenya wakitaja kukerwa na masuala ya ufisadi, ukosefu wa ajira kwa vijana, na mswada tata wa fedha ulitopiliwa mbali 2024.

OCCRP ni mtandao wa kimataifa wa waandishi wa habari wapekuzi ulioanzishwa mwaka wa 2006, maalumu kwa uhalifu uliopangwa na ufisadi.

Tangu 2012, OCCRP imetoa Tuzo ya ‘Mtu Bora wa Mwaka’ ili kutambua “mtu au taasisi ambayo imefanya mengi zaidi kupambana na uhalifu uliopangwa na ufisadi duniani.”

By Mjomba Rashid