Mamlaka ya kupmambana na utumiziz wa dawa za kulevya nchini NACADA imebaini kwamba zaidi ya asilimia 45 ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wametumia mihadarati katika kipindi fulani cha maisha yao.
Katika ripoti yake iliyowasilishwa Alhamisi, NACADA imeeleza kuwa zaidi ya ailimia 8 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni waraibu wa mihadarati na wanafaa kusajiliwa katika vituo vya ubadilishaji tabia.
Akizungumza mnamo Alhamisi wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo waziri wa usalama na masuala ya ndani Kipchumba Murkomen ametaja suala hilo kama suala sugu linalohitaji kukabiliwa kwa haraka.
Utafiti huo uliotelekelezwa katika vyuo 17 nchini umefichua kwamba matumizi ya bangi miongoni mwa wanafunzi nchi ni asilima 10 ambaayo ni mara tano zaidi ya asilimia ya watumiaji kote nchini.
Kadhalika imefichua ongezeko kubwa la matumizi ya shisha miongoini mwa Wanafunzi wa kike.
Prof. John Muteti ni Afisa Mkuu Mtendaji wa wa NACADA nchini.
“Asilimia 45.6 ya wanafunzi walikiri kuwa wametumia dawa au dutu moja vibaya maishani mwao. Miraa pia ilienea miongoni mwa wanafunzi (asilimia 10.1), muguka (asilimia 9.9), bangi iliyovuta sigara (asilimia 14.9) na bangi inayoliwa (asilimia 11.9).”
Sababu kuu za hatari ambazo zilihusisha wanafunzi kutumia dawa za kulevya ni pamoja na kushindwa kustahimili hali zenye mkazo, kiwewe cha utotoni ambacho hakijatatuliwa, Ukatili wa Kijinsia, kucheza kamari na kuwa na mpenzi wa kike au Kiume na kielelezo tayari kinachotumia dawa hizo.
Baadhi ya hatua za kupunguza zilizopendekezwa ni pamoja na huduma za mwongozo na ushauri, programu za ushauri, huduma nafuu za urekebishaji, ufuatiliaji wa wazazi na juhudi za uhamasishaji katika taasisi zote.
By Mohammed Mwajuba