HabariLifestyleNews

Angalizo! Huduma za Kununua Tokeni za Umeme Kukatizwa kwa Saa 24 Mwezi Juni

Kampuni ya umeme ya Kenya Power imetangaza kukatiza sehemu ya mfumo wa kulipia umeme kwa njia ya tokeni kwa saa 24 kwa ajili ya uboreshaji.

Wateja wamearifiwa kuwa mfumo ulioathiriwa hautaweza kufanya kazi kuanzia Jumapili Juni tarehe 2 saa nne usiku hadi Jumatatu ya tarehe 3, 2024 Juni saa nne usiku.

Katika kipindi hiki cha matengenezo wateja hawataweza kununua tokeni za umeme katika vituo vyovyote vya kuuza vikiwemo ofisi za Kenya Power, nambari zao za malipo za Mpesa, Airtel money na njia zote za benki.

Kenya power sasa imewataka wateja kununua token mapema ili kuepuka hitilafu hiyo iliyopangwa kutokea.

BY MJOMBA RASHID