HabariNews

Mawaziri Wateule Joho na Mvurya Washauriwa Kushirikiana Kulihudumia Taifa

Baadhi ya wakaazi kaunti ya Kwale sasa walimtaka  waziri mteule Salim

Mvurya na mwenzake  Ali Hassan Joho kushirikiana katika kuhudumia taifa
na kueka kando tofauti zao baada ya  kujumuishwa katika uteuzi wa
mawaziri katika wizara ya biashara  na uekezaji na ile ya madini na
uchumi samawati  mtawalia.

Wakiongozwa na Hamisi Juma  Shomali  walimpongeza rais Ruto kumrudisha
waziri Salim Mvurya ambapo wameitaja hatua hio kuonyesha heshima kubwa
kwa wakaazi wa Kwale na pwani nzima kwa ujumla .

“Wakati baraza la mawaziri lilipovunjwa  sisi kama wa Kwale tulikuwa
na   wasiwasi sana kwa maana   rais alipoteuwa upya  mawaziri kwa awamu
ya kwanza hakukuwa na mwakilishi kutoka eneo la pwani ,ila hadi sasa
tunampongeza rais kwa kumteuwa waziri Mvurya na mwenzake Ali Hassan Joho
hii ni heshima kubwa kwa wakaazi wa pwani ,” Asema Shomali .

Aidha Shomali alimtaka waziri Mvurya na mwenzake Hassan Joho kuhakikisha
wanaleta pamoja wakaazi wa eneo la pwani na Kenya Kwa ujumla.

“ Hatuwezi kueka taifa katika joto la kisiasa kila wakati ,tunataka
mawaziri wetu mueke kando tofauti zenu za kisiasa na muhudumie wakenya
kuambatana na kanuni za katiba ya nchi ,waziri Mvurya ujue sisi
tunajivunia kama wa Kwale na tunataka wakati mnaposherehekea baada ya
kuapishwa sherehe hio muifanye kwa pamoja hapa Kwale  ili wapwani  na
Kenya kwa ujumla wathibitishe umoja wenu.

Wakati uo huo alimsihi rais Ruto kuhakikisha  aliyekuwa waziri wa jinsia
Aisha Jumwa pia anapata nafasi kwa mara nyengine katika serikali ya
Kenya Kwanza .

“ Ikiwa nafasi itapatikana  rais umkumbuke  dada yetu  Aisha Jumwa na
pia unyoshe Zaidi mkono wako hadi kaunti ya Lamu na uteuwe kiongozi
,naamini bado kuna nafasi katika serikali yako ,” Asema Shomali.

Kwa upande wake  mfanyibiashara  Richard onsongo alimtaja waziri Mvurya
kama kiongozi ukakamavu anayejua majukumu yake katika kazi.

“Uteuzi wa waziri Mvurya ni haki yake mana hii serikali ya Kenya
Kwanza aliipigania ,kwa hio kuteuliwa kwake ni kwa halali na haki na
ninashukru rais kwa kumteuwa ,waziri Mvurya aliwafanyia kazi  wakaazi wa
Kwale kwa kipindi cha miaka kumi akiwa gavana ,hivyo nina Imani kuwa
wizara hii ya biashara na uekezaji pia ataiendesha kwa haki na uwazi
kama alivyofanya alipokuwa katika wizara ya madini na uchumi samawati
,”Asema Onsongo .

Aidha alimtaka waziri Mvurya kueka mwafaka wakuleta waekezaji Zaidi
nchini  kama njia mojawapo ya kufungua nafasi za ajira kwa vijana
hususan kaunti ya Kwale .

“ Hatuna waekezaji wakutosha na zaidi  katika kaunti ya Kwale na hatua
hio imewapelekea vijana kukosa ajira kote nchini  ,tukipata waekezaji
wakutosha  vijana wetu watapata ajira ili wajiendeleze kimaisha na
kuepuka vishawishi potofu ,” azidi kuelezea Onsongo

Kando na hayo alimtaka waziri wa madini na uchumi samawati Ali Hassan
Joho kufuata nyayo za waziri Mvurya  katika uendeshaji wa wizara hiyo.

“ Waziri Joho tunamuomba sana ushauriane  na magavana ambao kaunti zao
zina madini   ili  upate mwongozo wa jinsi shughuli za uchimbaji  na
sheria zinatekelezwa , hapa Kwale tuko na madini katika mlima wa Mrima
huko Lungalunga  kwa hio usikimbilie kuleta waekezaji na kuikandamiza
jamii inayoishi pembezoni mwa mlima huo ,ninataka uje ushauriane na
gavana Fatuma Achani kabla ya shughuli zozote za uchimbaji kutekelezwa
,achanganua zaidi Onsongo.

 
BY BINTIKHAMIS MOHAMMED