Wataalamu wa masuala ya Kawi kaunti ya Kilifi wameeleza haja ya Taifa la Kenya Kukumbatia uzalishaji wa kawi mbadala kufanikisha shughuli mbalimbali za kiuchumi hapa nchini.
Wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa kawi kaunti ya Kilifi Wilfred Kenga alieleza kwamba vyanzo vya nishati kwa sasa havina uwezo wa kuzalisha kawi ya kuwezesha viwanda kufanya kazi kwa saa 24 nchini.
Kulingna na mkurugenzi huyo ni kuwa huenda taifa likakosa kuafikia azma yake ya kuongeza kawi ya kutosha kulingana na ruwaza ya 2030.
Hii ni baada ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Nuclear eneo la Uyombo kaunti ya Kilifi kupata pingamizi kutoka kwa wakaazi na wanaharakati wa masuala ya mazingira.
Alisistiza kwamba ili Kenya ikuze Uchumi wake kwa kasi ya juu ni sharti fedha nyingi ziwekezwe kwenye masuala ya Kawi.
“Unaona ya kwamba nuclear ni katika kawi zile ambazo ukiiwasha inaeza kukupatia moto ambao unaeza kurun for 24 hours.
So within the Kenya vision 2030 for industrialization, you need nuclear in the energy mix, you need geothermal and you need hydro,” alieleze Kenga.
Kadhalika Kenga ameshikilia kwamba kawi ya nuclear ndio mfumo bora wa kawi wenye uwezo wa kufanya kufanikisha shughuli mballimbali akieleza haja ya kushughulikia uchafu wa unaotokana na kiwanda cha nuclear ili kuepusha madhara kwa viumbe hai wa ardhini pamoja na wale wanaoishi baharaini.
“Kila mmoja anavyo ambavyo analichukulia. Kwa sababu kuna the issue of nuclear waste which is very key ambayo environmentalist wamekuwa wakilalamika.
But mbali na the nuclear waste ambayo iko, the nuclear energy itself remains to be the most efficient and non-emmitance to the environmrnt.” Alisisitiza.
Miezi kadhaa iliyopita wakaazi wa uyombo walishiriki maandamano ya amani kupinga mradi huo baada ya kile kilichodaiwa kuwa maafisa wa mradi huo kuingia eneo hilo na kuanza ujenzi wa mnara.
Wakaazi hao wakiongozwa na wanaharakati wa mazingira waliutaja mradi huo kama wenye madhara makubwa.
Kulingana na wakaazi hao mradi huo wa kawi unalazimishwa kwao licha ya kuukataa kutokana na madhara yake.
BY EDITORIAL DESK