Masaibu ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza yanaendelea kumwandama baada ya Wawakilishi Wadi kaunti hiyo kumbandua ofisini.
Wawakilishi wadi 49 wamepiga kura ya kumwondoa uongizini kwa kile wanachodai ni utumizi mbaya wa ofisi na mamlaka yake miongoni mwa madai mengine.
Spika wa bunge la kaunti ya Meru Ayubu Bundi sasa ana muda wa saa 48 kumjulisha rasmi spika wa Seneti Amason Kingi kuhusu notisi ya kuondolewa madarakani kwa gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwangaza.
Kisheria Spika wa bunge la Seneti atawaarifu maseneta ndani ya siku saba kuhusu kuondolewa ofisini kwa gavana huyo, kisha bunge la seneti litakuwa na siku 10 kuchunguza madai yanayomkabali gavana Mwangaza na kutoa uamuzi dhidi yake kupitia kamati maalumu ya bunge hilo.
Aidha maseneta wote wa bunge la seneti wanaweza kushikiri katika kumbandua au kumrejesha ofisini kama ilivyofanyika awali baada ya kuchunguza madai yanayomkabili.
Hii itakuwa ni mara ya tatu sasa kwa Gavana huyo kubanduliwa ofisi katika kipindi cha miaka 2 tangu kuingia uongizini.
By Mjomba Rashid