Uncategorized

Mamia ya Wakazi Mvita-Mombasa Wajitokeza kwa Matibabu ya Bure

Wakazi wa Mombasa wameshauriwa kutenga muda wa kutembelea vituo mbalimbali vya afya kwa ajili ya ukaguzi wa afya zao.

Akizungumza wakati wa zoezi la matibabu ya bure eneo la Majengo eneobunge la Mvita Mwenyekiti wa Lulu ya Jamii, Lulu Hassan amesema wakazi wengi wanaugua maradhi mbalimbali lakini hukosa kutembelea vituo vya afya kujua hali zao.

Ameeleza kusikitishwa na idadi kubwa ya watu waliojitokeza katika matibabu hayo, akisema inaashiria kuwa kuna mamia ya watu ambao wanakosa kupata matibabu kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Naye Mrotari Anil Godha amesema idadi kubwa iliyoshuhudiwa hawakua wametarajia idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwa ajili ya matibabu hayo hivyo wataweza kupanga mipango zaidi ili kuweza kuwasaidia ambao hawajasaidika.

Kwa upande wao Wakaazi wa Mombasa hawakuficha furaha yao kutoka na msaada huo uliowapa afueni ya gharama ya matibabu huku wakiitaka serikali kuu kuhakikisha kwamba wanapunguza gharama ya maisha.

Haya yanajiri huku zaidi ya watu 500 eneobunge la Mvita waliojitokeza wakifaidika na matibabu ya bure iliyoandaliwa na Klabu ya Rotary kwa ushirikiano Wakfu wa Lulu ya Jamii, huku wakazi wakipata huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali kama vile kisukari, shinikizo la damu maradhi ya macho, miongoni mwa mengine.

By News Desk