HabariNews

Watu 6 akiwemo mtoto mchanga Waangukiwa na Ukuta na Kufariki Miritini-Jomvu

Watu 6 akiwemo mtoto mchanga wameaga dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa ua mtaani KCC-Miritini eneobunge la Jomvu kaunti ya Mombasa.

Watano hao walikuwa wamehudhuria hafla ya mazishi wakati mvua ilipoanza kunyesha na wakachukua hifadhi kuzijiba na mvua karibu na ukuta unaozunguka kiwanda kilicho karibu.

Afisa katika idara ya Dharura ya kaunti ya Mombasa, Ibrahim Basafar amesema kuwa mmoja kati watano hao alithibitishwa kufariki hospitalini Jomvu alikokuwa amepelekwa kupokea matibabu baada ya kujeruhiw vibaya.

Imeripotiwa kuwa mama mja mzito ni miongoni mwa sita hao walioaga dunia, ambapo Mtoto mchanga na wengine watatu walithibitishwa kuaga dunia papo hapo.

Waziri wa barabara na miundomsingi Dan Manyala aliyezuru eneo hilo ameagiza kubomolewa mara moja kwa sehemu ya ukuta iliyosalia huku akiagiza wawekeza wanaoendeleza ujenzi kuhakikisha wanafuata kanuni za ujenzi siku za usoni.

Miili ya watu hao imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani, Makadara uchunguzi ukianzishwa kutokana na mkasa huo.

By Mjomba Rashid