Habari

Matayarisho ya KCPE yakamilika…

Waziri wa elimu Professor George Magoha amesema kuwa wanafunzi wa darasa la nane wamekamilisha matayarisho ya mwisho kabla ya mtihani wao wa kitaifa kuanza rasmi jumatatu wiki ijao.

Akizungumza katika shule ya Kakamega, Magoha amesema wanafunzi waliolazimika kuhama shule zao kutokana na janga la mafuriko, watafanya mitihani yao,bila tashwishi.

Ameongezea kuwa, wizara yake inachunguza madai kwamba, baadhi ya shule za kibinafsi zilizokataa kuwasajili watahiniwa waliokosa kulipa ada ya kukalia mitihani, ya kitaifa.

Magoha amesema serikali iliwalipia ada ya mtihani wa kitaifa watahiniwa wote nchini, wakiwemo wa shule za umma, na wenzao wa shule za kibinafsi, na kila mwanafunzi, anafaa kukalia, mitihani hio.

Aidha, amepiga marufuku wanahabari na raia kutembelea maeoneo kunakoendelea mitihani ya kitaifa. Magoha, ameongeza kaunti ya Homabay kwenye orodha ya kaunti zinazomulikwa kuhusu wizi wa mitihani, kando na Migori, Kisii na maeoneo ya Isbania.

Watahiniwa takriban milioni moja nukta tisa tatu. 1.93, wamesajiliwa kufanya mtihani wao wa kitaifa wa KCPE, na KCSE, mwaka huu.