Kulingana na msimamizi wa hosipitali ya Kilifi Timothy Musau kusitishwa kwa huduma za chumba hicho ni kutokana na kuhamisha vifaa vya chumba hicho cha ya zamani hadi chumba kipya cha kuhifadhia maiti.
Hata hivyo wakazi wanaotaka huduma za chumba hicho sasa watalazimika kupeleka miili ya jamaa zao katika hifadhi ya maiti mjini Malindi na hosiptali kuu ya ukanda wa Pwani kaunti ya Mombasa.
Hatua hiyo haijapokelewa vyema na wafanyibiashara wa kutengeneza majeneza wanaosema kuwa kufungwa kwa hifadhi hiyo kutasambaratisha biashara zao.
Munga Shoboi ni kiongozi wa wafanya biashara ya majeneza.
Huduma hizo zinatarajiwa kurejelewa tarehe 14 mwezi Aprili.