AfyaHabari

Viwango vya chanjo ya Astrazeneca kuzuia maambukizi vyapunguzwa….

Kampuni ya Astrazeneca sasa imepunguza viwango vya uwezekano wa chanjo yake kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kwa asilimia 3.

Ripoti ya hivi punde inaonesha kwamba chanjo ya astrazeneca inazuia maambukizi kwa asilimia 76 wala sio 79 kama ilivyoripoti hapo awali.

Hata hivyo imesisitiza kwamba inazuia kwa asilimia 100 walioambukizwa dhidi ya kuzidiwa na ugonjwa na hata kufariki dunia.

Utafiti huo mpya unafuatia malalamishi kutoka kwa taifa la Marekani kwamba data iliyokuwa ikitumika ni ile ya kwanza wakati wa majaribio ya matumizi ya chanjo hiyo na utafiti mwingine ulihitajika kufanyika.

Chanjo ya astrazeneca ndio imeidhinishwa kutumika katika mataifa mengi duniani ikiwemo Kenya licha ya baadhi ya mataifa kulalamikia madhara yake.

Ikumbukwe kwamba shirika la afya duniani WHO limeendelea kusisitiza kwamba chanjo hiyo ni salama na kuyashauri mataifa kuendelea kuitumia.