Watahiniwa takriban 428 katika ukanda wa Pwani hawakuweza kukalia mtihani wao wa kitaifa wa KCPE.
Kulingana na mshirikishi wa elimu katika ukanda wa Pwani, Edward Arita, kaunti ya Mombasa pekee imerekodi idadi kubwa ya watahiniwa waliokosa mitihani hiyo.
Aidha miongoni mwa watahiniwa hao, 139 wametoka kaunti ya Mombasa huku 118 walitoweka katika kaunti ya Kilifi.
Hii ni baada ya kuripotiwa kuwa miongoni mwa watahiniwa waliotoweka, 59 ni wa kaunti ya Kwale, 48 Taita Taveta, 46 Tana River na 18 kutoka Lamu.
Hata hivyo, Arita amesema kuwa wizara ya elimu itaweza kuwapa watahiniwa hawa nafasi nyingine ili kuifanya mitihani hii.