Mkurugenzi wa WHO tedros amesema mwaka ulipoanza alitoa hakikisho kwamba katika kipindi cha siku mia 100 duniani kila taifa litakua limeanza kutoa chanjo kwa raia wake. Tedros amesema kwamba siku zimesalia 15 kwa kipindi hicho kukamilika huku mataifa 16 yakiwa hayajatoa chanjo hiyo.
Miongoni mwa maitaifa hayo 16 yanatarajiwa kuanza kupokea chanjo hiyo juma lijalo huku 20 yakiwa hayana mpango wowote wa kupata chanjo.Mkurugenzi huyo amesema kwamba mpango wa covax utayari kusambaza chanjo kwa mataifa yote maskn ila chanjo hiyo haipatikani.
Covax inalenga kusambaza chanjo milioni mbili kwa mataifa hayo katkia kipindi cha mwaka mmoja huku akiwashtumu mataifa tajiri kwa kujinunulia chanjo nyingi hivyo kusababisha nchi nyingine kukosa. ni wiki hii ambapo taifa la india lilitangaza kusitisha kwa muda usambazaji wa chanjo ya astrazeneca kufuatia ongezeko la maambukizi nchini humo uamuzi ambao WHO umeielewa.
Kulingana na repoti ya hivi punde ya WHO iliyotolewa siku ya jumanne ,Marekani inaongoza kwa utoaji chanjo ambapo asilimia 39 ya raia wake wamechanjwa ikifiuatwa na mataifa ya bara uropa ambapo wamechanja asilimia 14 na bara la afrika ikisalia nyuma kabisa ambapo idadi ya waliochanjwa ni asilimia 0.68.