Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka 2021 yanatazamiwa kutangazwa leo adhuhuri na waziri elimu profesa George Magoha.
Profesa Magoha anatazamiwa kumfahamisha rais Uhuru Kenyatta kwenye ikulu yake kabla ya kutoa matokeo hayo.
Matokeo ya mwaka uliopita yalilazimika kuhairishwa baada ya kalenda ya masomo kutatizwa na janga la covid-19.
Kutokana na ratiba iliopo, wanafunzi hao wanatazamiwa kujiunga na kidato cha kwanza ifikipo mwezi july mwaka huu.
Mtihani huo wa KCPE ulianza tarehe 22 hadi 24 machi mwaka huu ambapo Zaidi ya wanafunzi laki saba waliafanya mtihani huo.