Habari

Wakaazi Pwani wahimizwa kuchukua kadi zao za huduma…………

Wakaazi katika mkoa wa Pwani wameshauriwa kujitokeza kuchukua kadi za Huduma Namba baada ya kubainika kuwa asilimia kubwa ya kadi hizo bado hazijachukuliwa licha ya wenyewe kutumiwa jumbe fupi kwa njia ya simu.

Afisa mkuu wa usajili wa watu katika eneo la Pwani Aggrey Masai amesema licha ya kupeleka kadi hizo mashinani idadi ya wanaojitokeza kuchukua kadi hizo ingali chini.

Akizungumza mjini Mombasa Masai amesema ni muhimu kila mwananchi aliyejiandikisha kuchukua kadi hiyo itakayokuwa na taarifa zote muhimu kuhusu mtu binafsi.

Haya yanajiri huku baadhi ya wakaazi Mombasa wakisema  kufikia sasa  bado hawana ufahamu mwafaka kuhusu  jinsi kadi zitakavyotumika.

Wakazi wa likoni nao wanalalamikia ukosefu wa hamasa kuhusu zoezi la utoaji wa kadi hizo wakisema kuwa idadi kubwa kutoka eneo hilo hawana ufahamu kuhusiana na zoezi hilo.

Wakiongoza na mkereketwa wa masala ya jamii na siasa ambae pia amejitokeza kuwania kiti cha uwakilishi wadi katika wadi ya Bofu Paul Kinako, licha ya seriklai kutangaza kadi hizo zichukuliwa, wengi hawajui pakuenda kwani hawajapata ujumbe mfupi kwenye simu zao kama inavyodaiwa na serikali.

Aidha kinako ametoa wito kwa serikali kuja wazi katika kuelezea wakenya zoezi hilo kwani kuna baadhi ya waliokosa kujiandikisha katika awamu ya kwanza na  bado mpaka sasa hawajui kama kweli pia wao watapata nafasi ya kujiandikisha.

By Reporter David Otieno