Wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Kwale wamejitenga na madai ya kujihusisha na visa vya utovu wa usalama.
Wakiongozwa na Mohammed Abdallah, wamedai kuwa visa hivyo vinatekelezwa na wahalifu wanaotumia pikipiki zao.
Wahudumu hao wameeleza kwamba wakati mwingine wanashambuliwa na wahalifu hao wanaojifanya kuwa abiria.
Wakati uo huo, wamejiondolea lawama ya kuhusika katika visa vya kuwapachika mimba hasa watoto wa shule katika jamii.
Haya yanajiri baada ya takriban wahudumu elfu moja kujiunga na shirika la kijamii linalolenga kushughulikia changamoto zao.
By Correspondent Binti Khamis