Jamii ya wabajuni kutoka kaunti ya lamu inaitaka serikali kujitahidi kupambana na tatizo la dawa za kulevya eneo hilo.
Mkuu wa baraza la wazee wa Bajuni Omar Sharif anasema vijana wengi kaunti ya lamu wameathirika na utumizi wa mihadarati.
Anasema serikali inafaa kuhusisha jamii katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Naye daktari Othman Mujahid mshauri wa maswala ya usalama, amepongeza juhudi za shirika la save Lamu kuingilia kati ujenzi wa kiwanda cha mkaa wa mawe, akisema imesaidia jamii kuepuka madhara ya kimazingira.
Comment here