Habari

Idadi ya watahiniwa wa KCSE watakaojiunga na vyuo vikuu mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Idadi ya watahiniwa wa KCSE watakaojiunga na vyuo vikuu mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Watahiniwa elfu 17 zaidi wamepata alama ya kujiunga na vyuo vikuu katika matokeo yaliyotangazwa hapo jana.

Kwa mujibu wa waziri wa elimu proffesa George Magoha, ongezeko hili ni dhihirisho kwamba sekta ya elimu ilistahimili makali ya janga la corona, huku watahiniwa wengi nchini wakiendelea kusherekea matokeo bora huku shule nyingi zikirekodi matokeo mazuri ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Mtahiniwa kwa jina Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang’a ndiye aliyeibuka wa kwanza katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCSE nchini.

Wanjala amepata alama ya A ya asilimia 87.3 ,huku mwanafunzi wa pili akiwa Wesonga Allan aliyepata alama ya A ya asilimia 87.1 kutoka shule ya upili ya Agoro Sare huku watatu akiwa Sharon Cheong’eno kutoka shule ya upili ya Kenya High.

Waziri Magoha amewahakikishia kila mwanafunzi aliyefanya mithani  ya kitaifa wa kidato cha nne mwaka huu na kupata matokeo yake kuwa atapata nafasi ya kuendeleza masomo yake katika ngazi ya juu.

Magoha amesema serikali ya  kitaifa imeweka mikakati  dhabiti kufanikisha ajenda hiyo.