Mazingira

Kaunti ya Taita Taveta imetakiwa kushirikiana kwa kufuatilia miradi…

Kaunti ya Taita Taveta imetakiwa kushirikiana kwa kufuatilia miradi inayofadhiliwa na mashirika mengine kwa ajili ya faida ya wakaazi wa kaunti hiyo.

Wafugaji wa nyuki katika kaunti hii wamelalamika kuwa baadhi ya miradi inayoanzishwa na mashirika ya nje hukwama kutokana na serikali kukosa kushirikiana na kufuatilia miradi hiyo kuhakikisha kuwa inaendelezwa kufaidi jamii hii.

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji hao, Emmanuel Mwangoma ametoa wito kwa wizara ya kilimo na ufugaji kaunti hiyo kuwashika mkono wafugaji wa nyuki kupitia  mafunzo na  kuimarisha miradi ya ufugaji wa nyuki inayotekelezwa na mashirika mengine.

Kwa upande wake waziri wa kilimo, uvuvi na ufugaji kaunti hii Davis Mwangoma amewahakikishi wafugaji wa nyuki ushirikiano na juhudi za serikali ya kaunti kuimarisha ufugaji wa nyuki kama sehemu ya kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza mapato kwa wakulima.

BY FATUMA RASHID