Hisia zazidi kutolewa na viongozi wa miungano ya walimu , kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wa tume ya kuajiri walimu nchini TSC wa hivi karibuni akiwa ni katibu katika chama cha walimu KNUT tawi la Taita Taveta Lenox Mshila.
Kulingana na Mshilla amemtaja mwenyekiti mpya wa tume hiyo Jamleck Muturi kama mtu aliye na tajiriba ya uongozi , na hivyo kuteuliwa kwake kutaleta mwafaka kati ya tume hiyo na chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT.
Wakti huo huo katibu huyo amesema kuwa ni wakati walimu waanze kufaidika na chama hicho kwani kwa mda sasa wananchi wamekuwa na dhana kuwa chama cha KNUT na tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC, imekuwa ikikumbwa migogoro ya mara kwa mara.
Aidha Mshilla ameongeza kuwa iwapo walimu watawakilishwa kikamilifu na matakwa yao kusikizwa na serikali hata , matokeo ya mitihani kwa wanafunzi yatabadilika.
BY FATUMA RASHID