Wizara ya afya kaunti ya Kwale imebainisha kuwa watoto chini ya umri wa miaka 5 na wanawake wameathirika pakubwa na ugonjwa wa Malaria.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa afya ya jamii eneo la Matuga Kache Ndupha anayewataka wakaazi kulala ndani ya neti ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Nduva amedokeza kwamba wizara hiyo imetoa vyandarua vya kuzuia Malaria kufuatia ongezeko la visa vya ugonjwa huo kaunti ya Kwale.
Afisa huyo amewataka wakaazi kutumia ipasavyo vyandarua hivyo ili kuzuia vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria.
Nduva amewataka wenyeji kutunza vyandarua hivyo badala ya kuvitumia kuvulia samaki na kufanyia kazi zingine zisizofaa.
BY BINTIKHAMIS MOHAMMED