AfyaKimataifa

Chanjo dhidi ya Corona

Imebainika kwamba watu wengi duniani wako tayari kupokea chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Ripoti ya shirika la UGOF kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Imperial cha Uingereza imeonesha kwamba Uingereza ndiyo inayoongoza kwa asilimia 78, ikifuatwa na Denmark kwa asilimia 67.

Hata hivyo nchini Ufaransa asilimia 44 ya raia wake, wamesema hawako tayari kupokea chanjo hiyo.

Nchini Australia, Japana, Korea Kusini na Singapore idadi ya wananchi ambao hawana nia ya kupokea chanjo hiyo, imeendelea kuongezeka tangu mwezi novemba mwaka jana.

Utafiti huo ni miongoni mw tafiti zilizofanywa kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO ili kuelewa mienendo ya watu wakati wa majanga.

Tangu mwezi aprili mwaka jana, watu elfu 470 wamehojiwa kuhusu suala hilo, huku utafiti huo ambao ni wa hivi punde zaidi ukifanyika kati ya januaru tarehe 4 na tarehe 24.

Tafiti hizo zimebainisha kwamba watu wengi wanaamini chanjo huko wale wasioamini wakiwa ni asilimia 12 pekee.

Comment here