Mkereketwa wa maswala ya siasa na jamii ambae ni mshauri katika baraza la wazee wa bajuni Hassan Albeity amesema kuwa hawajaridhishwa na jinsi serikali kuu inavyoendesha shughuli ya mpango wa bandari ya lamu yani lapset akidai kuwa wakazi wa eneo hilo hawajahusishwa kikamilifu.
Akizungumza na meza yetu ya habari katika mahojiano ya kipekee hii leo Kiongozi huyo amesema kuwa licha ya serikali kutoa fidia kwa wanati wa kaunti hiyo hasa kwa wavuvu, fidia hizo hazitoshi kwani ingekuwa vyema serikali kuweka mikakati dhabiti ya kutafuta suluhu ya kudumu kwa wakazi hao.
Mwanasiasa huyo ameongeza kuwa licha ya wanati wa kaunti hiyo kupata nafasi katika bodi ya mradi huo bado kama walamu nafasi hiyo ni chache kwani kuna idadi ya vijana waliopelekwa shule kusomea taaluma ya uhabaria ambao kufikia sasa bado hawajahusishwa kikamilifu ,
Albeity aidha ameshutumu serikali kwa kukosa kuwalipia karo wanafunzi zaidi ya 1000 waliochukuliwa na seriklai ili kuwapa mafunzo watakaotumia katika bandari hiyo.
By David Otieno