Shirika la Kijamii la I choose Life Afrika limezindua mpango wa kutoa msaada wa vifaa vya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kwa wanafunzi wa shule za kaunti ya Mombasa.
Mkuu wa Shirika hilo Judy Manene anasema mpango huo uitwao “Jielimishe girls education Challange” utasaidia pakubwa kuzuia maambukizi ya covid 19 miongoni mwa wanafunzi wa shule 20 za upili.
Bi Manene anasema wamekuwa wakishirikiana na mashirika mbali mbali ikiwepo serikali katika kutoa msaada wa vifaa hivyo hata maeneo ya mashinani ikiwepo mpango wa kufadhili masomo ya kupitia mtandao.
Akizungumza hapa Mombasa Bi Manene amesema family 500 hapa Mombasa zimekuwa zikipata msaada wa fedha za kujikimu kimaisha kutokana na ugumu wa maisha unaosababishwa na virusi vya corona.
Amesema mpango wa kutoa ufadhili wa vifaa hivyo unaendelea kwa muda wa miezi 3.
Afisa mkuu wa idara ya watoto kaunti ya Mombasa Phillip Nzenge amesema mpango huo wa Jielimishe unatoa manufaa makubwa kwa wanafunzi wa shule kujikinga na maambukizi ya covid 19.
Comment here