Habari

KNUT yatishia mgomo wa walimu

Chama cha walimu nchini KNUT kimetishia kutangaza mgomo wa kitaifa iwapo tume ya kuajiri walimu nchini TSC haitaitisha kikao cha kujadili mkataba mpya wa nyongeza ya mshahara na marupurupu chini ya kipindi cha siku saba zijazo.

Kupitia barua kwa TSC, katibu mkuu wa KNUT Willson Sossion ametoa makataa hayo ya siku saba baada ya kulalamikia kupuuzwa kwa makataa mengie ya wiki tatu waliotoa awali.

Chama cha KNUT kinataka mkataba mpya wa kati ya mwaka 2021 na mwaka 2023 kuwekwa baada ya mkataba uliokuwepo kukamilika.

Wakati huo huo TSC badala yake imebatilisha uhusiano wake na KNUT, hatua ambayo imesababisha chama hicho kuendelea kudorora zaidi kifedha na kiidadi.

Ikumbukwe kuwa walimu walioko ndani ya muungano wa KNUT hawajakuwa wakinufaika na makubaliano ya awali ya nyongeza mishahara baada ya KNUT kushinda kesi mahakamani kuizuia TSC kutumia tathmini ya kazi ili kuwapa nyongeza hiyo.

Kufikia sasa matawi kadhaa ya chama hicho cha KNUT yamefungwa baada ya kushindwa kumudu kodi na hata mishahara ya wafanyikazi.

Comment here